JINSI YA KUONGEZA KIPATO

Uchumi.



Dunia ya leo ya mapinduzi ya nne ya viwanda ni tofauti na Dunia ya enzi za Ujima ambapo binadamu alitegemea kutembea kutafuta mahitaji yake kama matunda,mizizi na nyama kwa kuokota.

Kwenye Dunia ya leo inakuhitaji kuwekeza katika maarifa zaidi ,ambapo utafungua akili na kuona fursa na kuziendea na pia utahitaji kuanza kuwekeza .Uwekezaji una maana pana ingawa watu wengi hufahamu uwekezaji ni pesa pekee ambalo sio kweli.Uwekezaji ni sawa na kumwambia Fundi wa nguo ashone suti,fundi akiambiwa suti yeye hupata picha kamili kwenye akili yake kwahiyo fundi mpaka anatoa hiyo nguo basi tunasema nguo inayoonekana ni picha ya kilichomo ndani ya fundi.
Uwekezaji ni mawazo kwanza na ndio pesa hufuatia.

Namna ya kuongeza kipato
Kama nilivyo andika hapo awali kitu cha kwanza ni kuandaa mawazo sahihi ambayo ndio mtaji namba moja kwenye namna ya kuwekeza (kuongeza kipato).
_KUTUNZA ASILIMIA YA KIPATO UNACHOPATA:- Njia ya kuongeza kipato ni kutunza pesa kutokana na kipato unachoingiza kiwe cha siku,mwezi au mwaka .Mfano kila siku kama unapata elfu kumi (10,000) unatakiwa kutunza walau elfu 2,000 au hata elfu moja.Kutunza pesa kunahitaji nidhamu ya hali ya juu ambayo inakulazimisha ujinyime mambo ya anasa.Ukiweka malengo na kubadilisha fikra ni rahisi kuyafikia malengo yako.
_KUMILIKI CHANZO ZAIDI CHA KIPATO:-Watu wengi wakipata ajira ni rahisi kujisahau kwa kudhani ajira yao ndio kila kitu lakini ukweli kuajiriwa hakukupi kipato cha kutosha .Mfano wa kutokubali kuridhika na fedha za ajira ni kama mchezaji Cristiano Ronaldo  ,pamoja na kulipwa mabilioni ya shilingi kwenye vilabu vyake na matangazo anayoyapata kwenye dili zake lakini bado Ronaldo anamiliki mahoteli yake na biashara za mitindo pia.Kutegemea kipato cha sehemu moja ni kujitakiwa umaskini.
_KUONGEZA MUDA WA KAZI NA KUBANA MATUMIZI YASIYO YA LAZIMA:-Mfanyabiashara mkubwa Afrika Aliko Dangote huwa anafanya kazi masaa 20 kati ya masaa 24 ya siku nzima.Dangote anafundisha kuwa na muda mwingi wa kufanya kazi ,pamoja ni kwamba Aliko ni bilionea namba moja Afrika.
Kubana matumizi yasiyo ya lazima ni muhimu kwa sababu pesa inatakiwa kuongezeka na sio kupungua ,kwahiyo matumizi ya pesa ni vizuri kuyaangalia kwa jicho la tatu.

Pamoja na wengi kulalamika kuwa hakuna ajira na pesa ,wewe unatakiwa kuwa wa kwanza kukataa hali hiyo maana kisaikolojia utajiharibia namna ya kutafuta suluhisho la maisha yako mazuri.Jifunze kuona fursa na kuzifikia ubadili maisha yako .

Maoni

HABARI KUU LEO

GUARDIOLA AWAPIGA DONGO LIVERPOOL

YANGA NA ARSENAL ZAGAWA DOZI