Machapisho

CHELSEA YAICHAPA 4 BURNLEY

Picha
London Burnley wakisafiri kwenda mjini London kuifata timu ya Chelsea Fc wamepokea kichapo cha magoli manne bila majibu. Chelsea chini ya mkufunzi , Tomas Tuchel imejipatia magoli kupitia kwa     Reece James 47',Harvertz 52' 55" na Christian Pulsic 69". Urejeo wa James umeirejesha Chelsea kwenye makali yake maana winga huyo amefunga na kusaidia goli lingine. Chelsea wanasalia nafasi ya tatu nyuma ya Liverpool na Manchester city. Kwingineko, Liverpool imeichapa Westham goli moja kupitia kwa Sadio Mane. Matokeo mengine     Norwich 1-3 Brentford    Newcastle 2-1Brighton    Wolves 0-2 Crystal palace    Aston villa 4-0 Southampton

DRAKE ANUNUA NYUMBA YA NDOTO YAKE

Picha
Los Angeles. Rappa Drake wa nchini Marekani amenunua nyumba yenye thamani ya dola za marekani milioni 85 sawa na bilioni 187 za shilingi ya Tanzania. Nyumba hiyo iliyopo eneo la Beverly Hills mjini Los Angels nchini Marekani ina ukubwa wa futi za mraba 25,000 . Nyumba hiyo ina vyumba vya kulala 10,bafu za kuogea 22,gereji za magari 11,gym na viwanja vya mchezo wa tenisi.

RAIS PUTIN AOMBWA KUUA ZAIDI

Picha
  Moscow. Meja Jenerali wa Chechnya,  Ramzan Kadyrov  amemuomba Rais Vladimir Putin aruhusu mapigo mabaya ya kushtukiza ili Ukraine isalimu amri ndani ya muda mfupi wa masaa 24. Ramzan ambaye vikosi vyake viko vitani ameshauri kuachana na mapatano ambayo hayatakuwa na maana zaidi ya kusaini karatasi. Amesema hawezi kuvumilia kuona wanajeshi wake wanauawa na kadri wanavyozidi kuchelewa ndivyo wanakumbana na vikwazo zaidi.

Harmonize FT Bruce Melodie-TOTALLY CRAZY (Official Video)

Picha
 Msanii wa Bongo Fleva na mmiliki wa lebo ya KONDE GANG,Harmonize ametoa video ya wimbo wake aliomshirikisha Bruce Melodies hujulikanao kama "Totally Crazy). __ TAZAMA VIDEO