Machapisho

RAIS WA UKRAINE AKATAA KUIKIMBIA NCHI YAKE

Picha
Kiev. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amekataa ofa ya Marekani ya kumsaidia kuondoka Ukraine. Rais huyo amesema " mapambano yamefika,nahitaji risasi ,sio msaada wa kuondoka" Marekani na washirika wa Ukraine walikuwa tayari kumpa msaada Rais Zelensky kuondoka nchini mwake. Rais huyo ambaye amewahi kuwa mwigizaji wa majukwaani amekuwa Rais wa Ukraine tangu 2019.

KURASA ZA MAGAZETI JUMAMOSI YA 26/02/2022

Picha

ATHARI ZA VITA YA URUSI NA UKRAINE KWENYE MICHEZO

Picha
Dar es salaam. Vita ya Urusi na Ukraine ilioanza tarehe 23/02/2022 imezua sintofahamu kubwa duniani ambapo nchi nyingi zimeonyesha kutofurahishwa na hatua ya majeshi ya Urusi kuivamia na kuipiga Ukraine. Vita hii ambayo dunia inashuhudia haijaacha athari kwingine hata kwenye michezo athari zipo nyingi kama ifuatavyo:- Fainali za Uefa zabadilishwa: Fainali ya Uefa iliyotarajiwa kuchezwa 28 Mei kwenye uwanja wa St Petersburg imeamishiwa nchini Ufaransa kwenye uwanja wa     The stade de France uliopo mjini Paris. Manchester United imetangaza kuvunja mkataba wa udhamini na shirika la ndege la Urusi yaani     AEROFLOT ni baada ya majeshi ya Urusi kuivamia Ukraine. Timu za Serie A kukaa kimya dakika 5: Ligi ya mpira wa miguu ya Italia yaani Serie A itashuhudia kuanzia leo timu za Milan na Udinese zikikaa kimya kwa dakika 5 kama ishara ya kutaka amani ya UKRAINE. BUNDESILIGA yaweka mabango uwanjani: Usiku wa leo utashuhudia vilabu vya Stuttgart na Hoffenheim vikiingia uwanjani na mabango ya

RAIS VOLODYMYR ZELENSKIY WA UKRAINE ATAJA ATHARI ZA VITA NA URUSI

Picha
Kiev. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy ametoa taarifa ya athari za shambulio la Urusi kwa nchi yake huku akitaja jumla ya watu 137 kuwa wamepoteza maisha wakiwemo na wanajeshi 10 na mpaka sasa jumla ya majeruhi ni 316. Rais Volodymyr amenukuliwa " leo nimewauliza viongozi 27 wa nchi za Ulaya kuhusu kuhofia shambulizi la Ukraine lakini hakuna aliyejibu ,sisi hatuogopi ,hatuogopi chochote ,hatuogopi kuilinda nchi yetu,hatuwaogopi Urusi na hatuogopi kuongea na Urusi. Familia yangu ,watoto wangu wote ni raia wa Ukraine sio wakimbizi kulingana na taarifa tayari tuna maadui ambapo mimi ndio "target" yao ya kwanza na familia yangu ni "target" namba mbili .Wanataka kuimaliza ikulu"