Machapisho

RAIS VOLODYMYR ZELENSKIY WA UKRAINE ATAJA ATHARI ZA VITA NA URUSI

Picha
Kiev. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy ametoa taarifa ya athari za shambulio la Urusi kwa nchi yake huku akitaja jumla ya watu 137 kuwa wamepoteza maisha wakiwemo na wanajeshi 10 na mpaka sasa jumla ya majeruhi ni 316. Rais Volodymyr amenukuliwa " leo nimewauliza viongozi 27 wa nchi za Ulaya kuhusu kuhofia shambulizi la Ukraine lakini hakuna aliyejibu ,sisi hatuogopi ,hatuogopi chochote ,hatuogopi kuilinda nchi yetu,hatuwaogopi Urusi na hatuogopi kuongea na Urusi. Familia yangu ,watoto wangu wote ni raia wa Ukraine sio wakimbizi kulingana na taarifa tayari tuna maadui ambapo mimi ndio "target" yao ya kwanza na familia yangu ni "target" namba mbili .Wanataka kuimaliza ikulu"

RAYVANNY NA LOKOLE WAINGIA VITA YA MANENO

Picha
Dar es salaam. Mtangazaji wa kipindi cha Mashamsham cha Wasafi FM ya jiji Dar es salaam  Juma Lokole amejikuta kaenye ugomvi na msanii wa Bongo Fleva Rayvanny. Mtangazaji huyo wakati akitangaza alitoa ushauri kwa msanii Rayvanny kwamba alifanya makosa kwa kuachana na mzazi mwenzake Fahma na kuamua kuwa na mahusiano na mrembo Paula. Kutokana na ushauri huo Rayvanny naye alimjibu mtangazaji huyo kupitia Insta story akimueleza kwamba aachane nae kwasababu yeye na mzazi mwenzake bado wanaheshimiana. ___Zaidi Tazama video

BUSTA RYMES AMPA TANO DIAMOND PLATINUMZ

Picha
Dar es salaam. Msanii na mfanyabiashara kutoka code +255 namaanisha Tanzania,  Diamond Platinumz ameachia video na audio ya wimbo wake GIDI ambapo kupitia mtandao wa Instagram aliandika gidi is out of global . Kupitia ujumbe wake aliouweka kwenye Instagram ,miongoni ya walioweka maoni ni nguli rapa     Basta Rhymes alieweka emoji za moto zipatazo saba (7) kuonyesha kukubali kile anachofanya Diamond Platinumz . Wimbo wa Gidi huenda nao ukawa kwenye viwango vya wimbo wa jeje ambao umekuwa gumzo kwenye klabu nyingi za starehe nchini Marekani.

KURASA ZA MAGAZETI YA LEO 24/02/2022

Picha