Machapisho

ALIKIBA APATA PIGO KWENYE NDOA YAKE

Picha
Dar es salaam Msanii wa bongo fleva Alikiba amepewa siku 15 za kwenda kujitetea katika kesi inayomkabili. Kesi yake ambayo imefunguliwa na mke wake Amina Khalif kwenye mahakama moja mjini Mombasa Kenya imemtaka staa huyo kufika kutoa maelezo kabla ya uamzi wa kuvunjwa kwa ndoa ya wawili ao. Amina mapema mwaka huu aliitaka mahakama hiyo kuridhia kuvunja ndoa ya wawili hao huku ikitajwa kwamba familia ya Alikiba wamekuwa wakimnyanyasa mrembo huyo raia wa Kenya na pia Alikiba ameshindwa kumjali mke wake .

KURASA ZA MAGAZETI YA LEO

Picha

JINSI YA KUJIPATIA HELA KUPITIA MTANDAO WA FACEBOOK

Picha
BIASHARA. Mtandao wa kijamii wa Facebook ni mmoja ya mitandao mikubwa ya kijamii duniani ukiwa na takribani watumiaji bilioni 4. Mtandao huu unaomilikiwa na kampuni ya META iliopo chini ya bilionea kijana Mark Zuckerberg. Mtandao huu ni miongoni mwa mitandao ya kampuni hii ya META ambayo pia inamiliki Whatsapp ,   Instagram na Messenger. NAMNA YA KUTENGENEZA PESA FACEBOOK Facebook kama ulivyo mtandao wa kibiashara huwa unatoa fursa ya watumiaji wake kunufaika na mtandao huu. Hili utengeneze pesa kwanza fungua 1)  Facebook page: Eneo hili upatikana kwenye kushoto mwa ukurasa wa facebook. -Baada ya kufungua page ,vutia watu kwa kuomba wajiunge na page yako.Page yako itahitaji watu elfu moja (1000) tu hili kuthibitishwa. -Anza kuweka video:Facebook wanalipa kwa video yako tu na wala sio picha,kadri video yako inavyotazamwa ndio huwa unatengeneza pesa ambako watu elfu moja (1k) wakitazama video basi kuanzia hapo video yako itaanza kulipwa.     Mambo ya kuzingatia unapoweka video kwenye Fac

Rais MWINYI APONGEZA TEKNOLOJIA YA KUPIMA CORONA "EDE COVID SCANNER"

Picha
Zanzibar. Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa Zanzibar imekuwa ni nchi ya kwanza Afrika kutumia teknolojia ya mashine ya kupima UVIKO (EDE COVID SCANNERS) kutokana na azma yake ya kuimarisha sekta ya utalii ambayo ndio tegemeo kubwa la uchumi wa Zanzibar  Rais Dkt Mwinyi aliyasema hayo leo wakati akifanya mahojiano na waandishi wa habari wa kimataifa na kitaifa kufuatia matukio makubwa yaliyotokea leo hapa nchini katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume likiwemo kuanza tena kwa safari za ndege ya "Fly Dubai" kutoka umoja wa nchi za kiarabu (UAE) ,pamoja na uzinduzi wa matumizi ya mashine ya (EDE COVID SCANNERS) ya kupima UVIKO 19. Alisema kuwa hatua hiyo itapunguza matatizo ambayo wasafiri wanayapata na kusisitiza kwamba ni muhimu serikali kufanya kila juhudi katika kurudisha watalii hapa Zanzibar ambapo ndege ya "Fly Dubai" itakuwa inakuja mara mbili kwa siku.