YANGA YAKAA MGUU SAWA UBINGWA LIGI YA TANZANIA

Dar es salaam.



Mzunguko duru la kwanza la ligi ya NBC PREMIER LEAGUE umemalizika leo kwenye uwanja wa Manungu Complex ukishuhudia wababe wa Dar es salaam timu ya wananchi Yanga wakiwachapa Mtibwa Sugar magoli mawili (2) bila majawabu.

Mchezo huo uliokuwa wa mwisho kwenye ufungaji wa mzunguko wa kwanza wa ligi uliitimishwa kwa magoli ya Saido Ntabazonkiza (45+) na Fiston Mayele (67) na kuihakikishia Yanga kukaa kileleni mwa ligi ikiwa na pointi 39 ikifuatiwa na Simba Sports club yenye jumla ya pointi 31.

Wakati mzunguko wa kwanza unamalizika imeshuhudiwa mchezaji wa timu ya Namungo 


  Reliants Lusajo akiongoza kwa kuziona nyavu huku akiwa na magoli 7 akifatiwa na Mwaikenda na 


  Mayele wote wakiwa na jumla ya magoli 7.Mpaka sasa jumla ya michezo 120 imechezwa huku jumla ya magoli yakiwa ni 228.

Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea kuanzia tarehe 27/02/2022 kwa hatua ya raundi ya pili ya michuano hiyo ya ligi ya NBC.


Maoni

HABARI KUU LEO

GUARDIOLA AWAPIGA DONGO LIVERPOOL

YANGA NA ARSENAL ZAGAWA DOZI