MKE WA BILIONEA MSUYA AKIRI KUMUUA WIFI YAKE

Dar as salaam.

Mke wa aliekuwa mfanyabiashara maarufu wa madini mkoani Arusha ,marehemu Erasto Msuya ,Miriam Mrita ameeleza sababu na namna alivyohusika na mauaji ya wifi yake Aneth Msuya.






Miriam ambaye ni mshtakiwa wa kwanza katika kesi ya mauaji hayo ya wifi yake huyo Aneth aliyeuawa mei 25,2016 kwa kuchinjwa shingoni akiwa kwake Kibada Kigamboni ,jijini Dar es salaam amekiri kuhusika na mauaji hayo katika maelezo yake.

Katika maelezo hayo,Miriam ameeleza kuwa aliamua kumuua wifi yake kwasababu alikuwa anamfuata fuata katika suala la usimamizi wa mirathi ya mumewe marehemu bilionea Msuya na kwamba katika kutekeleza mauaji basi alimkodi mtu aliemlipa sh 20 milioni.

Mbali na Miriam mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo namba 103 ya mwaka 2018 inayosikilizwa na Jaji Edwin Kakolaki Mahakama kuu kanda ya Dar es salaam ni mfanyabiashara Revocatus Myella.



Maelezo hayo ya Miriam yalisomwa mahakamani hapo na shahidi wa kwanza wa upande wa mashtaka,WP sajenti Mwajuma ,aliyemhoji mshtakiwa huyo na kuandika maelezo yake alipotiwa mbaroni baada ya kupokewa mahakamani hapo kuwa kielelezo cha ushahidi wa upande wa mashtaka.

Kwa mujibu wa maelezo hayo mshtakiwa huyo aliteuliwa kuwa msimamizi wa mirathi ya marehemu mumewe , Bilionea Msuya ambaye aliacha wosia kuwa asilimia 40 ya mali alizoacha benki wapewe wazazi na dada zake na asilimia 60 za mali wapewe mke na watoto wake.



Pia,marehemu bilionea Msuya alieleza katika wosia huo kuwa mali nyingine zilikuwemo magari ,mgodi na hoteli zilipaswa kugawanywa kwa utaratibu wa mirathi.

Maoni

HABARI KUU LEO

GUARDIOLA AWAPIGA DONGO LIVERPOOL

YANGA NA ARSENAL ZAGAWA DOZI