JIFUNZE NAMNA YA KUMPATA MME NA MKE HAPA

Dar es salaam.


Suala la mahusiano limekuwa na changamoto sana kutokana na wengi wanaoingia kutokuwa na uelewa wa jambo lenyewe.

Mahusiano yana changamoto ambazo upelekea watu kuwa na visasi ambavyo uzaa vifo,talaka na watoto wa mitaani.

Mbinu za kupata Mme na Mke hizi hapa
1.Mtangulize MUNGU :Hapa lazima pawe ni kipaumbele kwasababu mwanzilishi wa ndoa ni MUNGU mwenyewe na ndio anaunganisha watu pia.

2.SHIRIKISHA MTU UNAEMWAMINI: Watu wa kwanza wa kukuletea Mme au Mke ni wazazi wako au mlezi.Wazazi au walezi wanapokuchagulia mke au Mme wao wataangalia mambo haya;-
A)Mila na desturi. Mzazi au mlezi ana uelewa wa suala la ndoa kwahio masuala ya tamaduni atayaangalia .Mchagga atataka kijana au binti amuoe au aolewe na Mchagga mwenzake kwasababu atajua mila na desturi ni kiungo sahihi kwenye ndoa.
B)Tabia.Historia ya wazazi wa binti au kijana wataifatilia ambayo huwa inaakisi tabia za binti au kijana anaengia kwenye ndoa.

3.CHAGUA MTU AMBAYE NI WA AINA YAKO.Vijana wengi hili wanalijua kwa juu juu ,hapa unatakiwa kuangalia mpenzi ambaye ana kipato mnaendana au kwa mwanaume kipato kiwe zaidi ya mke na pia mwanaume unatakiwa uwe na sifa zaidi ya mke kwasababu wewe ndio unatakiwa kuwa kichwa.

4.EPUKA KUTANGULIZA KIGEZO CHA KIPATO NA UZURI.Mabinti wanatamani kuolewa na watu wenye pesa nyingi ambazo hawafahamu wenza wao walizipataje? Kwenye ndoa ni lazima muanze hatua zote kuanzia chini ndio heshima inakuepo.Vijana nao uangalia mabinti warembo,sio vibaya lakini kigezo cha kuoa kisiwe tu uzuri bali MTU ambaye atakuwa msaidizi kweli kwenye ndoa.Ndoa inahitaji mwanaume awe kichwa na mwanamke awe msaidizi.

5.CHAGUA MTU UTAKAEMPENDA DAIMA.Upendo ni neno dogo lakini lina maana kubwa ambapo hata uvumilivu ukaa ndani yake.Unapooa au kuolewa na MTU unaempenda ni kwamba utamvumilia katika hali zote.Kwa wanawake ni jambo la kawaida kwasababu wanawake ni wavumilivu hata kama wenza wao wanapitia kwenye hali ngumu za kimaisha kama Afya na Uchumi.

Maoni

HABARI KUU LEO

GUARDIOLA AWAPIGA DONGO LIVERPOOL

YANGA NA ARSENAL ZAGAWA DOZI