AJINYONGA NA KUACHA KICHANGA CHA MIEZI MITATU

GEITA.



Katika hali isiyokuwa ya kawaida ,mwanamke mmoja aliejulikana kwa majina ya Naomi Ilyumba (22) mkaazi wa mamlaka ya mji mdogo Katoro Geita katika mkoa wa Geita amekutwa amejinyonga kwenye choo.



Afisa mtendaji wa kata ya Katoro bw Selemani Maushi amekiri kutokea kwa tukio hilo.Mwanamke huyu alijinyongea kwenye nyumba ya wageni ijulikanayo kama Mwananzoka inayomilikiwa na Siki Mwananzoka ambaye pia alikuwa ni mme wa bi Naomi.

Katika hali ya kuhuzunisha Naomi amejiua huku akiacha mtoto mchanga wa miezi mitatu (3) na huku chanzo cha kujiua kikitajwa ni wivu Wa mapenzi.

Maoni

HABARI KUU LEO

GUARDIOLA AWAPIGA DONGO LIVERPOOL

YANGA NA ARSENAL ZAGAWA DOZI