SABABU ZILIZOIONDOA GSM KWENYE MPIRA WA TANZANIA

Dar es salaam.


Taarifa ya kushtua kwenye mpira wa Tanzania imetoka leo ni baada ya kampuni ya GSM kuamua kukaa pembeni kama mdhamini mwenza wa mpira wa miguu Tanzania.

T


  aarifa ya Afisa mkuu wa biashara wa GSM Allan Chanjo imesema ,wao kama wadhamini wanajitoa kuwa wadhamini wenza wa ligi ya NBC PREMIER LEAGUE.Taarifa za GSM kujiondoa kwenye udhamini zinajiri ikiwa ni miezi miwili na wiki mbili tangu waingie mkataba na TFF novemba 23 2021.



Wakata sakata hili likijiri TFF imethibitisha kupokea taarifa ya GSM na kuahidi kutoa ufafanuzi baadae.Kupitia mazungumzo na kituo cha WASAFI RADIO  ,mmoja wa viongozi kwenye bodi ya ligi bw Kizuguto amekiri kupokea taarifa pia kutoka kwa katibu mkuu wa TFF.

Udhamini wa GSM ulipata nakama kwa siku za mwanzoni baada ya klabu ya SIMBA FC kutaka maelezo zaidi juu ya mkataba wa udhamini wa TFF na GSM ambako Simba kupitia kwa mtendaji mkuu wake


   Barbara walikataa jezi za Simba kuchapwa nembo ya GSM .

Taarifa za ndani kutoka chanzo kimoja zimethibitisha kuwa toka GSM achukue udhamini wenza mnamo Novemba 23 ya mwaka 2021 alikuwa hajatoa pesa yoyote .

Wakati huo bilionea Ghalib Said Mohammed amejiuzulu kwenye kamati ya mashindano ya Taifa stars



Maoni

HABARI KUU LEO

GUARDIOLA AWAPIGA DONGO LIVERPOOL

YANGA NA ARSENAL ZAGAWA DOZI