Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni, 2022

LIVERPOOL YAMNASA KINDA HUYU

Picha
Klabu ya Benifica ya nchi Ureno imethibitisha kuwa mshambuliaji wao Darwin Nunez kwa sasa ni mali ya Liverpool  ya nchini Uingereza. Klabu hiyo ya majogoo Liverpool imetoa kitita cha milioni 100 paundi za Uingereza hili kumsajili kinda huyo mwenye umri wa miaka 22 kwa kandarasi ya miaka sita (6). Liverpool  inajivunia uwepo wa wachezaji vijana kama Eliot (19),Carvalho (19),Nunez (22),Trent (23),Konate (23),Diaz (25) na Jota (25).

Shakira na Pique ndoa yao basi

Picha
Madrid, Hispania. Mchezaji wa Fc Barcelona Gerald Pique ameripotiwa kuachana na mke wake Kipenzi Shakira ambaye ni mama wa watoto wake wawili. Shakira kupitia marafiki zake amethibitisha kuachana na mmewe Gerald Pique.Ndoa ya wawili hao imedumu kwa miaka 11 .Ndoa ya wawili hao iliingia doa baada ya Gerald Pique (35) kuonekana na mwanamke mwingine katika mgahawa mmoja majira ya usiku ,hatua hii ilimkasirisha Shakira (45) ambaye amekiri mumewe alimsaliti. Shakira ni mwanamziki na pia mwanamitindo wa muda mrefu huku Gerald Pique  akiwa ni mchezaji mwandamizi kwenye klabu ya Fc Barcelona.

SABABU YA SADIO MANE KUONDOKA LIVERPOOL

Picha
Dar es salaam. Wiki hii huenda ikawa imepita vibaya kwa wapenzi na mashabiki wa  Liverpool  duniani ni baada ya vyombo vya habari kuripoti tetesi za mshambuliaji Sadio Māne kutaka kuondoka. Gazeti la  Daily star , la nchini Uingereza liliripoti uwepo mkubwa wa msenegali huyo kutaka kuondoka kwenye viunga vya Anflied baada ya klabu hiyo kushindwa kufikia makubaliano mapya ya kimkataba na fundi huyo mtupia magoli. Liverpool  mpaka sasa wanamlipa Mane kiasi cha pauni za Uingereza ,takribani laki moja kwa juma kwa mkataba wa sasa unaoisha msimu ujao wa mwaka 2023.Aidha, Sadio Mane amekuwa katika wakati mgumu kutokana na klabu hiyo kushindwa kumpa mkataba mpya ambao alihiitaji kiasi cha pauni laki mbili kwa juma sawa na     Mohammad Salah ambaye amepewa mkataba mpya na Liverpool kutoka ule wa zamani ambao amekuwa akivuna pauni 100000 kwa juma. Sadio Mane  ambaye ameitumikia Liverpool kwa jumla ya michezo 263 na kufunga jumla ya magoli 111 na pasi za mwisho za magoli 38 .Amefanikiwa kuwa ku