Machapisho

ENRIQUE UTATA MTUPU

Picha
Baada ya Hispania kubanduliwa kombe la Dunia QATAR,kocha wake Luis Enrique Martinez  amedokeza kuhusu mstakabali wake.   "Wiki ijayo nitazungumza hilo lakini kwasasa ni mapema,lla ni Mimi natakiwa kuwajibika" ENRIQUE ameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari waliotaka kufahamu iwapo atatangaza kuachia ngazi baada ya kufungwa na Morocco.

AFRIKA YAWEKA HISTORIA QATAR

Picha
Timu ya Morocco imekuwa timu ya Afrika mwaka 2022 kutinga robo fainali ya kombe la Dunia QATAR akiwafunga Hispania kwa mikwaju ya Penati. Mchezo huo ambao umedumu kwa takribani dakika 120 na nyongeza 8 umetamatika kwa Waarabu hao wa Kaskazini mwa Afrika kutakata kwa kuibandua Spain kwa mikwaju 3 bila majibu. Kijana aliezaliwa Madrid ndiye amekuwa gumzo kwa kushindilia mkwaju mkali wa mwisho wa Penati huku kipa wa Morocco akicheza mikwaju yote ya Marco Asensio,Laporta na nahodha wa Uhispanyola Sergio Busquet. Morocco atamsubiri mshindi kati ya Ureno na Uswizi hili atafute tiketi ya kwenda nusu fainali.

LIVERPOOL YAMNASA KINDA HUYU

Picha
Klabu ya Benifica ya nchi Ureno imethibitisha kuwa mshambuliaji wao Darwin Nunez kwa sasa ni mali ya Liverpool  ya nchini Uingereza. Klabu hiyo ya majogoo Liverpool imetoa kitita cha milioni 100 paundi za Uingereza hili kumsajili kinda huyo mwenye umri wa miaka 22 kwa kandarasi ya miaka sita (6). Liverpool  inajivunia uwepo wa wachezaji vijana kama Eliot (19),Carvalho (19),Nunez (22),Trent (23),Konate (23),Diaz (25) na Jota (25).

Shakira na Pique ndoa yao basi

Picha
Madrid, Hispania. Mchezaji wa Fc Barcelona Gerald Pique ameripotiwa kuachana na mke wake Kipenzi Shakira ambaye ni mama wa watoto wake wawili. Shakira kupitia marafiki zake amethibitisha kuachana na mmewe Gerald Pique.Ndoa ya wawili hao imedumu kwa miaka 11 .Ndoa ya wawili hao iliingia doa baada ya Gerald Pique (35) kuonekana na mwanamke mwingine katika mgahawa mmoja majira ya usiku ,hatua hii ilimkasirisha Shakira (45) ambaye amekiri mumewe alimsaliti. Shakira ni mwanamziki na pia mwanamitindo wa muda mrefu huku Gerald Pique  akiwa ni mchezaji mwandamizi kwenye klabu ya Fc Barcelona.