MORRISON ALICHOMFANYIA BOSS WAKE BARBARA HIKI HAPA

Dar es salaam.

Klabu ya Simba imemsimamisha winga wake mghana Bernad Morrison kutokana na utovu wa nidhamu.



Kupitia taarifa rasmi ya klabu hio iliotolewa na meneja wa mawasiliano Ahmed Ally ,imethibitika mchezaji huyo alimtolea maneno machafu CEO wa klabu io Barbara Gonzalez .



Timu ya Simba ilijipatia ushindi wa magoli 6 dhidi ya Dar City kwenye michuano ya kombe la shirikisho.Baada ya mchezo na timu ya Dar City ,Mtendaji wa klabu hio aliingia vyumba vya kubadilisha nguo ambako alimkumbatia mchezaji Clatos Chota Chama huku mchezaji Morrison nae akitaka kumkumbatia Barbara lakini CEO huyo alikataa hali iliopelekea Morrison kumwambia "acha shobo kwa 


Chama".Baada ya kauli hio ambayo Morrison aliisema kwa kiswahili ilizua sintofahamu kati ya viongozi na mchezaji huyo.

Simba ambayo kwa sasa inashika nafasi ya pili ya ligi ya NBC TANZANIA huku ikikabiliwa na ratiba ngumu ya mechi za kombe la shirikisho barani Afrika zitakazolindima mfululizo ndani ya mwezi huu wa pili.

Maoni

HABARI KUU LEO

GUARDIOLA AWAPIGA DONGO LIVERPOOL

YANGA NA ARSENAL ZAGAWA DOZI