Machapisho

WACHEZAJI WAPOKEWA KIBINGWA

Picha
Tokyo. Timu ya Taifa ya Japan maarufu"SAMURANBLUE" imewasili katika uwanja wa Ndege wa Narita Tokyo na kupokewa na maelfu ya watu. Wababe hao wa Asia walitolewa kwenye hatua ya 16 bora na Croatia baada ya kufungwa kwa mikwaju ya Penati 3 kwa 1. Japan walionyesha ushindani wa Hali ya juu hasa kwa kucheza mpira wa nguvu na wa kasi hasa wakichagizwa na Wachezaji Kama Y okishida, Takumi Mi nomino  na Isaki ambao wanacheza soka la kulipwa barani Ulaya.

KURASA ZA MBELE ZA MAGAZETI LEO

Picha
Magazeti ya Jumatano ya leo.

ENRIQUE UTATA MTUPU

Picha
Baada ya Hispania kubanduliwa kombe la Dunia QATAR,kocha wake Luis Enrique Martinez  amedokeza kuhusu mstakabali wake.   "Wiki ijayo nitazungumza hilo lakini kwasasa ni mapema,lla ni Mimi natakiwa kuwajibika" ENRIQUE ameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari waliotaka kufahamu iwapo atatangaza kuachia ngazi baada ya kufungwa na Morocco.

AFRIKA YAWEKA HISTORIA QATAR

Picha
Timu ya Morocco imekuwa timu ya Afrika mwaka 2022 kutinga robo fainali ya kombe la Dunia QATAR akiwafunga Hispania kwa mikwaju ya Penati. Mchezo huo ambao umedumu kwa takribani dakika 120 na nyongeza 8 umetamatika kwa Waarabu hao wa Kaskazini mwa Afrika kutakata kwa kuibandua Spain kwa mikwaju 3 bila majibu. Kijana aliezaliwa Madrid ndiye amekuwa gumzo kwa kushindilia mkwaju mkali wa mwisho wa Penati huku kipa wa Morocco akicheza mikwaju yote ya Marco Asensio,Laporta na nahodha wa Uhispanyola Sergio Busquet. Morocco atamsubiri mshindi kati ya Ureno na Uswizi hili atafute tiketi ya kwenda nusu fainali.