Machapisho

KURASA ZA MAGAZETI LEO MEI 9

Picha

GUARDIOLA AWAPIGA DONGO LIVERPOOL

Picha
Manchester. Kocha wa Manchester City na raia wa Hispania Pep Guardiola ameipiga kijembe klabu ya Liverpool  kuwa haina uzoefu na kubeba kombe la ligi ya Uingereza kwasababu ndani ya miaka 30 wamebeba kombe moja. Pep ametoa kauli hiyo baada ya timu yake kuichapa klabu ya Newcastle kwa jumla ya magoli 5 na kukaa kileleni mwa ligi ya EPL kwa jumla ya alama 86 baada ya kuingia dimbani mara 35 sawa na Liverpool ambae anashika nafasi ya pili akiwa amekusanya alama 83. Aidha, Pep ameisifia Liverpool kwa kupambana vizuri kwenye ligi ya mabingwa ulaya yaani UEFA ambako tayari wako fainali pamoja na Real Madrid.

SIMBA YAICHAPA RUVU SHOOTING 4-1

Picha
Ligi kuu ya NBC imeendelea leo kwa kuzikutanisha timu za Simba sc na. Ruvu shooting stars kwenye dimba la hayati Benjamini Mkapa. Simba akiwa ni mwenyeji wa mchezo huo amemfunga Ruvu shooting magoli manne(4) kupitia kwa Kibu Denis,Raly Bwalya,John Bokko na Enock Inonga huku goli pekee la RUVU limefungwa na Haruna Chanongo. Katika michezo mitatu yaani ya Kombe la Azam na Ligi kuu , Ruvu imefungwa jumla ya magoli 14.Kwa matokeo ya leo sasa Simba Sc anafikisha alama 46 na michezo 22 akishikiria bado nafasi ya pili nyuma ya Yanga Fc mwenye alama 56 kwenye kilele cha NBC PREMIER LEAGUE. Aidha stori kubwa kwa mchezo wa leo ni goli la Nahodha wa Simba John Rafael Bokko ambaye amefunga goli lake la kwanza msimu huu.

MOZEY BROWN - AGGY (Official Music Video)

Picha