HISTORIA YA MUIMBAJI LATA MANGESHKAR


Makala.



Mnamo tarehe 06/02/2022 saa 2:15 usiku katika hospital ya SANDWICH ndipo gwiji Lata Mangeshkar aliaga dunia huko Mumbai India huku dalili zote zikionyesha alikuwa na UVIKO 19 ulioshadidishwa na ugonjwa wa mapafu yaani Nimonia.Taarifa ya Dkt Patel Samudanh aliekuwa anamuangalia takribani siku 19 kabla ya kifo chake.Kwa mujibu wa daktari huyo ,viungo vyote vya mwili wake vilisimama na kukataa kufanya kazi ilipofika saa 2:12 usiku uo wa februari 06 mwaka huu.

Lata Mangeshkar  alikuwa muimbaji wa nyuma ya pazia (playback singer) ambaye kwa takribani miongo saba (7) mtawalia alitawala masikio na nyoyo za wapenzi wa filamu za kihindi maarufu Bollywood duniani kote.
Katika utamaduni wa filamu za kihindi,waimbaji huwa hawaimbi kama tuonavyo bali Casett uwekwa na muigizaji ujifanya tu kuimba kumbe sio kweli na uo ndio utamaduni wa wahindi mpaka leo.
Sauti yake Lata Mangeshkar waliemuita kifupi Lata G hutumika kama mvuto wa hisia kwa wapenzi wa filamu za kihindi ambao huusisha makabila ya kihindi 32 na rahaja inayoongelea taifa la Hindi.

Mangeshkar aliathiri soko la vijana wote na wanasiasa nchini mwake .Alizaliwa Mumbai India Septemba 1929 akiwa ni mtoto wa kwanza kwenye familia ya watoto watano wa Dinaganth na Benegath Mangeshkar .

Mangeshkar amezoa tuzo zote za umahiri kwenye fani ya mziki duniani sio India pekee mpaka nje ya nchi yake.Baba yake alikuwa mwimbaji wa  mziki wa asili yaani Indian classical ujulikanao kama Marat .Mzee huyu alifariki Lata akiwa na miaka 13 tu.
  • Lata anamuelezea baba yake "naweza kusema kipaji ni asilimia 75 na mafunzo ni asilimia inayobaki .Bila mafunzo sauti yako haiwezi kukusaidia kitu.Baba yetu alikuwa fundi wa  mziki wa asili wa kihindi unaitwa Marath.Mimi na ndugu zangu Asha na Usha alitufundisha ujuzi ,matamshi sahihi ,matumizi ya pumzi na sauti.Familia yote ilikuwa ni familia ya mziki lakini pia tulilithi ingawa baba akukusudia tuwe waimbaji wa kutoka hadharani .Kwakweli baba asingefariki Mimi nisingekuwa muimbaji,asingeruhusu maana mtoto wa kike katika mila zetu analindwa sana na jamii .Baba alikuwa mhafidhina sana hakuwa na mchezo ,sisi tulikuwa na nidhamu kubwa mno ."

Sauti yake Lata g ilikuwa ya mvuto wa aina yake na yenye upeo wa kipekee.

Lata Mangeshkar amewahi kufika Afrika Mashariki ,Kenya mnamo mwaka 1970 na alifanya onyesho kubwa mjini Nairobi na alifanikiwa kuimba wimbo wa kiswahili uitwao Malaika.


Maoni

HABARI KUU LEO

GUARDIOLA AWAPIGA DONGO LIVERPOOL

YANGA NA ARSENAL ZAGAWA DOZI